Kutokana na wilaya ya Makete kuwa miongoni mwa wilaya "Ngumu" hasa kimazingira na kibarabara pia, magari haya yameonekana kuwa mkombozi kwa watumiaji, kutokana na kufika sehemu mbalimbali ambazo magari mengine hayawezi kufika hasa wakati wa masika
Hapa ni Bulongwa ambapo gari hili aina ya Land Rover 109 limrnaswa na kamera yetu likipiga mzigo kwa kubeba kokoto licha ya barabara nyingi kuwa hazipitiki wakati huu wa masika, lakini hili linapita bila wasiwasi wowote.(Picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog)



