KIJANA AUAWA KWA KUPIGWA JIWE KUBWA KICHWANI BAADA YA KUWADHULUMU WENZAKE PESA ZA MAUZO YA ALMASI


Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mihangwa Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze Matelu kata ya Mwadu- Luhumbo tarafa ya Mondo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa baada ya kupigwa kwa jiwe kubwa kichwani na watu anaodaiwa kuwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya tukio hilo limetokea jana (Mei 7,2014) saa moja asubuhi katika kijiji hicho cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu.

Imedaiwa chanzo cha mauaji hayo  inasadikiwa  kuwa marehemu  amewadhulumu  wenzake watatu pesa za mauzo ya madini ya almasi.

Tayari jeshi la polisi mkoani Shinyanga  linawashikilia watuhumiwa wa mauaji hayo akiwemo Makoye Manyenze aliyesababisha kifo cha Mihangwa Maguta.

Watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa na polisi ni Abdalah Idd (32) na Ally Omary (22) wote wakiwa ni wakazi wa  kijiji cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo