KAMATA KAMATA YA BAJAJ NA PIKIPIKI KATIKATI YA JIJI LA DAR YAGEUKA DILI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWUx3sLmGezsJF9AffFMiHpB4H0xF2UgeGZPduYRaWzEmJUjioTUlExkOUvU47JLekbij4EfOpiLdwqRmxTvVtK7ZbGlkhsVPrQhapHYEhDrW4ipzIaVEwmz6k2inP91PNGbk-YG0FmEkp/s1600/unnamed.jpg 
Baadhi ya madereva wa pikipiki wanaozitumia kama vyombo vya usafiri binafsi  kwenda na kurudi kazini wakihoji juu ya mkanganyiko huo katika ofisi za  Jiji la Dar es Salaam, juzi. Hata hivyo hawakupata majibu zaidi ya  kukuta tangazo lililositisha upokeaji wa toza za kuingia mjini na  vibali.
======
 ZOEZI la kupiga marufuku bodaboda na bajaji zinazofanya biashara katikati ya  Jiji la Dar es Salaam limegeuka biashara kwa Halmashauri ya Jiji la Dar  es Salaam hasa kwa watumiaji wa pikipiki hizo kwa ajili ya usafiri  binafsi wa kawaida kwenda na kurudi kazini, pamoja na makampuni  yanayotumia chombo hicho cha usafiri.

Halmashauri ya jiji sasa imeanza kuwatoza watu binafsi na makampuni yanayotumia  chombo hicho shilingi 500 kwa siku kila bodaboda inapoingia mjini  wakidai ni tozo ya chombo hicho kupata idhini ya kuingia mjini kwa kila  siku.

Wakizungumza na mtandao huu jana baadhi ya wananchi wamelalamikia kitendo cha  Halmashauri ya Jiji kugeuza zuio la kufanya biashara ya bodaboda  katikati ya jiji aina ya biashara ya kujipatia fedha kwa kutoza shilingi mia tano kwa siku kwa kila pikipiki za watu binafsi na makampuni  zinapoingia mjini.

Mkazi wa Jiji, Jackson Chalamila alisema tayari amelipia kibali cha miezi  sita yaani shilingi 90,000 kama tozo ya kuingia mjini kila siku na  ameruhusiwa kuingia mjini na pikipiki yake anayodai huitumia kama chombo cha usafiri kwenda na kurudi kazini kila siku za kazi.

"...Binafsi nimelipia kutokana na usumbufu ambao ninaupata toka kwa mgambo wa jiji  kila siku wanatukamata ukiwaonesha kitambulisho cha kazi kinachokuonesha kuwa wewe hufanyi biashara ya bodaboda hawakitambui na wanasema  unatakiwa kuwa na kibali, hivyo nikalazimika kukata baada ya kulipia  shilingi 90,000," alisema Chalamila.

Aliongeza kuwa hata hivyo utaratibu huo si wa haki bali ni namna ya kuwanyonya  wananchi kwani mtu hawezi kulipishwa tozo za kuingia mjini kwa chombo  anachokitumia kama usafiri wake wa kwenda na kurudi kazini, ilhali  magari hayalipi tozo yoyote ya kuingia mjini.
"Huu ni utapeli mtupu, sisi tunalipa kodi kama ilivyo kwa magari binafsi na  ni chombo cha moto mtu unakitumia kama usafiri wako iweje ulipishwe kila siku unapoingia mjini? Mbona watu wanaotumia magari kama usafiri  binafsi hawalipi wanapoingia mjini? Huu ni wizi...," alisema.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijaR8TMYD9FgZHfxMpFuPI4-EW9l43CklXKtf6eRmUcqau4lKAfw8388aIImgnrWRDmGDziBpFhhW17f4LrHQnNLEPYBYazepFWdslHOx_VmY9XkpTYpVw2ZVFjhrBXyhS7q3zmL32-Hhl/s1600/unnamed+%281%29.jpg 
Mwandishi wa habari hizi alifika hadi ofisi ya Jiji kutaka kupata ufafanuzi juu  ya malalamiko hayo ya baadhi ya wafanyakazi wanaotumia pikipiki kwa  ajili ya shughuli zao binafsi na kutozwa ushuru wa kuingia mjini, lakini haikufanikiwa kumpata msemaji wa jiji ambapo walizi walidai ametoka nje ya ofisi kikazi.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia tangazo lililowekwa na Jiji la kuwarifu  wananchi kuwa limesitisha malipo ya tozo za pikipiki kuingia mjini hadi  hapo itakapotangazwa tena, ili kutoa nafasi kwa jiji kukagua vibali  vilivyotolewa na kuvihakiki kabla ya kuendelea. Hata hivyo baada ya  mkanganyiko huo baadhi ya watu waliolipia walianza kufika katika ofisi  hizo wakitaka kurejeshewa fedha zao na wengine kuhoji kadhia hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo