MTOTO mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.
Akipia stori na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema
anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zote, awe
anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi
mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi
au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alisema Jokate.
