DR. CHENI NAYE ALAZWA HOSPITALI KUTOKANA NA UGONJWA WA DENGUE



Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelazwa toka jana katika hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa Dengue.

Akizungumza nasi  leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
 
“Bado ni nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa,napungukiwa damu,mwili unauma,kwahiyo yanai bado ninaumwa,hii homa ilinianzia wiki iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana ndio wameingundua,” ameongeza.
 
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio mzuri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo