Mpaka sasa video hii imetazamwa zaidi ya mara laki moja na elfu 30
kwenye mtandao wa Youtube toka ianze kuonyeshwa April 29 2014 ikiwa ni
video ya kipekee na ya kiwango kingine cha juu tofauti na ilivyozoeleka
kwa Sauti Sol.
Mtandao wa Kenya ghafla.co.ke umeripoti kwamba imefahamika video hii
imezuiwa kuchezwa kwenye TV stations mbalimbali za Kenya kwa sababu
imevunja maadili.
Kwenye Mdundo Awards jana usiku Bien Aime wa Sauti Sol alisema
mwanasheria wao anashughulikia ishu ya kufungiwa kwa video yao ambayo
imeambiwa inachochea ngono kutokana na uwazi wa wanaookenana ndani yake.
Hii itakua video nyingine iliyochukua headlines zinazofanana na ile
ya P Unit ‘you guy’ ambayo ilifungiwa na CITIZEN TV kwa sababu ya mrembo
alieliachia umbo lake kwa sana.
Hata hivyo kwenye tuzo za Channel O 2013 P Unit walisema ‘video yetu inaonyeshwa sana bado na hata waliosema wameifungia ndio
wanatuita hapo kwa interview…, hii ni ile video mzazi wako anakwambia
usione alafu yeye usiku anaitazama’
tazama hapo chini
