Kero ya barabara za halmashauri ya wilaya ya Makete zilizoharibika kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha wilayani hapo inatarajiwa kumalizika baada ya halmashauri hiyo kutangaza kuwa barabara hizo zitaanza kukarabatiwa muda wowote kuanzia sasa
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu hivi karibuni Bw. Jackson Mahenge kutoka idara ya Ujenzi Makete amesema idaya hiyo imejipanga vizuri kuanza matengenezo ya barabara hizo ambapo kwa sasa mvua zinatarajiwa kumalizika mwezi huu mwishoni na baada ya hapo matangeneo yataanza
Amesema kwa sasa tayari wameshatangaza zabuni na wakandarasi kupatikana na kusaini mikataba ya kuanza matengenezo ya barabara hizo na kazi itaanza muda wowote kuanzia sasa mara baada ya mvua kumalizika
Orodha ikionesha barabara zitakafanyiwa matengenezo.
"Kwa mfano kumekuwa na malalamiko ya barabara hapa Makete mjini, ile ya kuelekea Tanesco, kama orodha hii ya barabara zitakazokarabatiwa, hapa makete mjini barabara zote zitafanyiwa matengenezo hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi, na orodha hii inaonesha barabara zote zitakazokarabatiwa" amesema Mahenge
Ameongeza kuwa pamoja na matengenezo hayo watakayoyafanya barabara hizo haziwezi kudumu kama wananchi hawatashirikiana pamoja kuzilinda ikiwemo kuzuia matumizi mabaya yanayoweza kuziharibu mapema kama kutozibua mifereji ya kupitishia maji pindi inapoziba katika baadhi ya maeneo na vingine kama hivyo
Katika msimu huu wa masika wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya ambazo barabara zake zilizopo chini ya halmashauri ziliharibiwa na mvua, hivyo baada ya mvua hizo kumalizika wataanza kuzifanyia matengenezo