GARI LA FREEMAN MBOWE LAKAMATWA NA POLISI NCHINI KENYA

Ni magazeti kadhaa ya leo Tanzania ambayo yameripoti kuhusu kukamatwa kwa gari la Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe huko Mombasa Kenya.

Jambo leo wameripoti kwamba gari la Mbowe lililokamatwa ni lile la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo limekamatwa kwenye msako wa magaidi na uhalifu nchini humo na Polisi wanamsubiri Mbowe na Wenje kwa mahojiano.
Screen Shot 2014-05-01 at 1.58.14 PM 
Gazeti la habari leo limeandika kwamba gari la Mbowe lashikiliwa Mombasa, namba mbili za STK na KUB zatisha Polisi Kenya na dereva ahojiwa akihisiwa kuhusika na ugaidi.

Uhuru wameandika shangingi la Mbowe lakamatwa Kenya, alikwenda huko na Ezekia Wenje, dereva wake ahojiwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo