Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la
Summry T.799 BET,Paul Njilo mkazi wa jijini Dar-es-salaam aliyegonga
askari polisi wanne na wananchi 14 na kusababisha vifo vyao.
Ajali
hilo imetokea aprili 28 saa 2.45 usiku katika babara kuu ya
Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Utaho tarafa ya Ihanja wilaya ya
Ikungi mkoani Singida.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, SACP,Geofrey Kamwela amesema kwa
sasa wanaendelea na taratibu za kisheria na watakapomaliza pamoja na
upelelezi,dereva Paul atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayomkabili.
Katika
hatua nyingine, Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia tiketi ya
CHADEMA,Tundu Lissu,ameahidi kutoa msaada wa kisheria kwa ndugu
waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya basi la summry.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Mungaa (CHADEMA) Mtheo
Alex wakati akizungumza kwenye hafla ya sala maalum ya kuombea watu 14
wakazi wa kijiji cha Utaho waliogongwa na basi la summary.
Amesema
mbunge huyo anatafuta nafasi ili afike kijijini hapo kutoa pole kwa
wafiwa na vile vile atashughulikia taratibu zote za fidia
zitakazotokananabimwa ya basi hilo T.799 BET mali ya kampuni ya summry.
“Taratibu
za bima huwa si za kumalizika kwa muda mfupi,kawaida huwa za muda
mrefu,kwa hiyo ndugu zanguni,kwa hili tuwe wavumilivu na tuendelee
kuamini kwamba mwanasheria wetu Tundu,atalimudu”,amesema.
Wakati
huo huo, Diwani wa kata ya Kituntu (CCM),Naftali Gwae alikanusha uvumi
kuwa rais Jakaya Kikwete alituma rambai rambi zikiambatana na fedha.
“Rais
wetu alituma salamau za rambi rambi na wala sio fedha.Kwa hiyo ndugu
zangu niwasihi tu kwamba wakati huu mgumu unaoambatana na majonzi,mengi
yatasemwa lakini tuwe makini na kuyafanyia uchunguzi kwanza”,amesema.
Aidha,uvumi
ulioenea kwamba Diwani wa CCM na Mtendaji wamechukua kutoka ofisi ya
kijiji nyaraka za benki zinazodaiwa kuonyesha kuwa kijiji hicho kina
akaunti yenye zaidi ya shilingi milioni mia moja,si za kwelei ni uongo
mtupu.
Kwa
mujibu wa Diwani Gwae baada ya sala hiyo,waathirika wa ajali hiyo kila
moja amepewa shilingi 212,500 ikiwa ni rambarambi kwa kupoteza
ndugu.
Fedha hizo ni kutoka fedha za ubani za shilingi 5 milioni
zilizotolewa na mmiliki wa kampuni ya summry,shilingi laki moja mkuu wa
mkoa wa Singida na shilingi 150,000 zilizotolewa na wakazi wa kijiji cha
Minyinga.
