BALOZI WA MALAWI NCHINI TANZANIA AFARIKI DUNIA

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKTVoQe8S30ebUXmaBHVKCfwh94z2HCiNIZyMYF3Y5ygi-iPsuuedxp6Cke9n_WgOUmM7HLjkeNu7ASTrmRNkw1lKJU7eLVbvRNBUgzv6yyt8prXXq6g9m6urzG-V1OOnUr_1P973h0wkM/s1600/lake+nyasa+072.jpg
Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga  (pichani) amefariki dunia leo jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

“Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.
 
“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo