ATELEKEZA PIKIPIKI ILIYOKUWA IMEBEBA NYAMA YA NYATI MARA BAADA YA KUWAONA POLISI MKOANI MBEYA

Nyama ya Nyati Imekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mbeya yenye uzito wa kilo 300 ikiwa inasafirishwa kwa kutumia Pikipiki yenye namba za usajili T.494 CDF aina ya T better.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani hapa Ahmed Msangi amesema kuwa limetokea Aprili 29 saa tisa alasiri katika kijiji cha Igawa,Kata ya Lugelele Tarafa ya Rujewa Wilayani Mbarali, Barabara kuu ya Mbeya kwenda Njombe na hatimaye Mtuhumiwa alikimbia na kutelakeza pikipiki yake mara baada ya kuwaona askari wa Doria

Kamanda Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na uwindaji haramu kwani ni kinyume cha sheria badala yake Wafuate Taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi pia kuomba kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hilo azitoe ili akamatwe na sheria ichukuliwe dhidi yake au ajisalimishe mwenyewe

Kwa sasa mtuhumiwa anaendelea kusakwa na jeshi hilo.

Na Saimen Mgalula wa Eddy blog Mbeya


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo