Kumtumia mtu ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini Kenya kunaweza kukuweka mashakani.
Maafisa wakuu wanasema kuwa yeyote atakeyepatikana na hatiaatafungwa jela kifungo cha miezi mitatu kwenda chini.
Afisa mkuu kutoka tume ya kitaifa ya
mawasiliano, Christopher Wambua ameambia vyombo vya habari nchini humo
kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono pamoja na picha
zenye watu walio uchi watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au
dola miatano na themanini na nane kama faini au kufungwa jela..
Onyo hilo litawaandamana hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya mkononi au kwenye internet.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango
ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za
watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za,
smartphone ilipanda hadi asilimia sitini.sexting
