MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Shija Machiya (30), mkazi wa Kijiji cha Butulwa, Kata ya Old Shinyanga alizua kizaazaa, baada ya kupanda kwenye nguzo ya umeme ya njia kuu inayopeleka umeme mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama.
Machiya alipanda katika nguzo hiyo inayosafirisha umeme wa msongo wa KV 220 katika eneo la Ihapa jirani na Kiwanda cha Nyama na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.Tukio hilo lilitokea saa5 asubuhi, ambapo wakazi wa eneo hilo waliacha shughuli zao kwa muda wakifuatilia tukio hilo pamoja na kuhofia maisha mtu huyo.Mama mzazi wa Machiya, Mondesta Madirisha, alisema kuwa kwa
“Mimi
nilikuwa nikitokea shamba, ghafla nilikutana naye akikimbia mbio.
Nilimsemesha na kumwomba asimame, lakini alikataa na kukimbilia
kulipokuwa na watu wakilima. Niliwaomba msaada wamkamate, lakini
aliwazidi mbio na hapo hapo aliamua kupanda katika nguzo ya umeme na
kwenda juu kabisa, ndiyo huko mlipomuona.”
Alifafanua
kuwa baada ya kuona hali hiyo waliamua kutoa taarifa kwa viongozi wa
Serikali ya kitongoji na kijiji, ambao waliliarifu Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), waliofika katika eneo la tukio, kisha kuwasiliana na
Polisi pamoja watu kikosi cha zimamoto.
Juhudi
za kumshusha kijana huyo kwenye nguzo hiyo zilifanyika huku Machiya
akirajibu kukwepa kwa kupanda juu zaidi ya nguzo, ambapo pia aliamua
kuvua nguo zake zote.
Hata hivyo Tanesco kushirikiana na Zimamoto walifanikiwa kumshusha kijana huyo bila madhara yoyote.
Akizungumzia
tukio hilo, Mhandisi wa Njia Kuu za Umeme mkoani Shinyanga, Job Bidya
alisema kuwa kitendo hicho cha Machiya kupanda katika nguzo za umeme
kingeweza kuhatarisha uhai wake kutokana na njia hiyo kupitisha umeme
mkubwa wa msongo wa KV. 220.
Alisema
kuwa baada ya kupata taarifa za tukio hilo, walilazimika kuzima umeme
na kufika eneo hilo kisha juhudi za kumteremsha kijana huyo zilifanyika
kwa ushirikiano wa kikosi cha zimamoto na uokoaji Manispaa ya Shinyanga,
Jeshi la Polisi na wananchi.
Jeshi
la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba kijana huyo anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi ili kujua iwapo
alifanya kitendo hicho kwa kuchanganyikiwa au kwa makusudi.