WANANCHI WILAYANI MAKETE WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA HAKIMU WA WILAYA

 Mwendesha mashitaka akitoa taarifa ya kutofika hakimu hii leo
 Wananchi wakisikitika kwa taarifa hiyo.
Wakianza kuondoka.
 wananchi wakiondoka baada ya kuahirishwa kwa kesi zao.
Wananchi wenye kesi mbalimbali katika mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wameiomba serikali kuwaonea huruma na kuwapatia hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo ili kupunguza tabu wanayoipata kuhusu uendeshaji wa kesi zao. 

Wameyasema hayo hii leo katika mahakama ya wilaya ya Makete wakati wakiahirishiwa kesi zao kwa sababu ya hakimu anayeendesha kesi zao kuwa na majukumu mengine ya kikazi yaliyplelekea kushindwa kufika.

Ikumbukwe kuwa wilaya ya Makete kwa hivi sasa haina hakimu wa wilaya na kesi zote zinaendeshwa na hakimu kutoka mahakama ya wilaya ya Njombe ambaye pia anaendesha kesi nyingine katika mahakama yake. 

Wananchi hao walioongea na mwandishi wetu kwa masharti ya kutotaja majina yao wamesema wengi wao wanatoka kata na vijiji vya mbali na mahakama hivyo kesi zinapoahirishwa mara kwa mara kwa sababu ya hakimu kushindwa kufika ama kupata udhuru imekuwa ikiwaumiza na kuwaongezea gharama.

"Unakuta ninafika hapa siku moja kabla ya kesi, na mimi natoka Matamba, kuja hapa sina ndugu lazima nilale kesho yake ndiyo nihudhurie mahakamani, ukija unaambiwa hakimu ameshindwa kufika kwa sababu mbalimbali, tunaahirishiwa kesi, sasa nadhani tungekuwa na hakimu wetu ambaye analala hapa hapa kesi zote zingekuwa zinaendelea kila siku kama zilivyo za mahakama ya mwanzo" amesema mwananchi mmoja. 

Awali akitoa taarifa ya kuahirisha kesi zote za mahakama ya wilaya mwendesha mashtaka Gosbert Komba amesema wamepewa taarifa ya kuahirishwa kesi zote za mahakama ya wilaya kutokana na hakimu kupata udhuru hivyo kushindwa kufika mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo