SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA BW. PHARS MSIRIKALE




Familia ya Bw. Phars Msirikale (Nyanda) inapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi kwa hali na mali katika msiba wa baba yetu mpendwa Mzee Msirikale. 

Asanteni kwa sala na michango yenu Mungu awarudishie mara dufu pale mlipotoa. Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu na apumzike kwa amani. Amina. 

Marehemu mzaa Msirikale alipata ajali ya gari manamo 6/04/2014 majira ya saa mbili asubuhi na kupelekwa hospitali teule DDH ambapo alipoteza fahamu lakini tarehe 8 ya mwezi huu ilionekana alihitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi na ndipo alipewa rufaa na kuhamishiwa hospitali ya rufaa Bugando Mwanza na kufanyiwa uchunguzi uliobaini kuwa alipata tatizo kichwani na damu kuvujia ndani. 

Kwa bahati mbaya mnamo  tarehe 12 mwezi huu majira ya saa 10 jioni aliaga dunia na kuzikwa 15 mwezi huu, marehemu apumzike kwa amani


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo