Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium
Muhemu akifafanua kwa waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa
hiyo katika kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo
rasmi pamoja na watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa
Manispa hiyo Bi. Joyce Nsumba. (Picha zote na FRANK MVUNGI-maelezo).
Afisa
Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha kuwa kanuni na
taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa
kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kujikinga na magonjwa
ya milipuko.
======= ====== ======
Na Hassan Silayo-MAELEZO.
Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa
mazingira kwa kuwa jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia
kanuni za usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa
ya Temeke Bw. Willium Muhemu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam.
Bw. Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka
mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za
usafi wa mazingira zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha
mlipuko wa magonjwa.
“Moja ya mikakati iliyowekwa na manispaa
ya Temeke ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo
yasiyo rasmi ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu
huo atachukuliwa uchafuzi wa mazingira” Alisema Bw. Muhemu.
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo
Bw. Ernest Mamuya alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa
katika hali ya usafi wakati wote wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya
kubeba taka , kuwa na dampo la kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka
zinazolewa kwa wakati. Akitoa wito kwa wananchi Bw. Mamuya
alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia kanuni za usafi katika ngazi za
familia ili kuunga mkono mpango wa manispaa katika utunzani wa mazingira.
Maafisa afya wa kata wanaendesha zoezi
la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya
za mitaa husika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.

