SAKATA LA MWALIMU MKUU KUFUNGUA BAA SHULENI, MAPYA YAIBUKA



 Baada ya siku chache kugundulika kuwa Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Unenamwa kata ya Luwumbu wilayani Makete Mkoani njombe anauza pombe za kienyeji na viwandani kwenye nyumba ya shule hiyo hali hiyo imethibitishwa leo na wananchi wa kijiji hicho

Wakizungumza katika mkutano uliofanywa na Mratibu wa Elimu kata ya Luwumbu Bw.Burton Mbedule wamesema kuwa ni kweli Mwl.Mkuu wa shule ya Msingi Unenamwa Evaristo Maginga amefungua kisiri kilabu cha kuuza Pombe za kienyeji na viwandani katika nyumba ya shule hiyo 

Katika Mkutano huo mratibu elimu kata Bw.Mbedule aliwataka wananchi wa kijiji hicho kumthibitishia taarifa hizo kama ni kweli kwani amesema yeye aliposikia taarifa hiyo alimuona Mwenyekiti na kuzungumza naye kuhusu uvumi huo,baada ya hapo alikutana na mwalimu huyo ambapo alimwambia mratibu huyo kuwa anataka anataka uthibitisho wa watu waliokuwa wanapata huduma hiyo kwake

Baada ya hapo amesema aliwatafuta wananchi kabla ya kuitisha Mkutano huo ambapo wananchi walimweleza kuwa taarifa za mwl.huyo kutengeneza pombe ni kweli na si kuuza pombe eneo la shule 

Bw.Mbedule Alipowataka wananchi kumthibitishia taarifa hizo katika Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa kijiji Bw.Labson Tweve wananchi wamesema kuwa huwa wanajipatia huduma hiyo katika nyumba hiyo hata kwa Oda na sio uongo kwamba huduma hiyo haipo shuleni hapo kwani wamekuwa wakiipata nyumbani hapo

Akizungumza na Kitulo fm Mwl. huyo siku ya Alhamisi wiki iliyopita katika kipindi cha Morning power alikana taarifa hizo na kusema kuwa kuwa yeye anauza vitu vidogovidogo na si Pombe

Hata hivyo wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya Msingi Unenamwa wameeleza kukerwa na elimu duni itolewayo na walimu waliopo shuleni hapo kwani wamekuwa wakikagua madaftari ya watoto wao na kusema ni tofauti na wanafunzi wanaosoma katika shule jirani kama Idende

Hivyo baadhi yao wamelazimika kuwahamisha watoto wao katika shule hiyo na kuwapeleka shule nyingine ya Idende kwa kuhofia watoto wao kupata elimu Duni kwani  endapo wakipelekwa Sekondari watakuwa na Uelewa Mdogo

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema hawajapendezwa na tabia ya walimu wa shule hiyo kwani wanafunzi wamekuwa wakifanya vibarua muda wa masomo kutoka Unenamwa hadi Mwakavuta kitu ambacho kinaongeza kufeli kwa wanafunzi kitaaluma

Hatma ya Mkutano huo wananchi wamemtaka Mratibu Elimu wa kata hiyo kuzungumza na Mwl.huyo na kumuonya mara moja aache biashara hiyo katika eneo la shule.
 
Na Furahisha Nundu via Kitulo Fm blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo