Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake
kuhusiana na ujenzi wa hatua za awali za bandari ya Kabwe,wilayani
Nkasi mkoani Rukwa.
Mmiliki
wa Kampuni ndogo ya
Kusindika samaki Bwa.Nassor Shibib,akimpa malezo mafupi Ndugu Kinana
namna ya kuhifadhi samki aina ya Migebuka kabla ya kusafirishwa na
kuuzwa katika nchi ya Zambia,Congo,Burundi na Rwanda na wafanyabiashara
wa eneo la Kabwe.
Ndugu
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ndogo ya Kusindika
samaki Bwa.Nassor Shibib,katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi,namna
ya kuhifadhi samaki kabla ya kuuzwa katika nchi ya Zambia,Congo,Burundi
na Rwanda na wafanyabiashara wa eneo la Kabwe.
Ndugu Kinana akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na suala la uvuvvi katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kujengwa bandari
Katibu
Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiangalia samaki katika kiwanda kidogo
cha kuhifadhia samaki na kuuza katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi
mkoa wa Rukwa mapema leo,ambapo pamoja na mengine Ndugu kinana alifanya
mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 21 katika
mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma,ziara hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha
Uhai wa chama,kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya CCM.
Samaki
aina ya Migebuka ikiwa imeandaliwa kwa ajili ya kukaushwa kabla ya
kuhifadhiwa kwenye majokofu na kusafirishwa maeneo mbalimbali,ndani na
nje ya nchi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Nkasi
Kaskazini,Mh.Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe
katika hatua za awali na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi
zinazofanyika katika kijiji hicho kabwe.
Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo jioni.
Katibu
Mkuu wa CCM;ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Kirando,wilayani Nkasi mapema leo.Kinana alisema kuwa tahakikisha
Barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kabwe
itatengenezwa kwa kiwango cha lami."Nitaenda na mbunge wenu kushinikisha
suala la barabara hii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na
kuwarahisishia sughuli za kibiashara"alisema.Alisema kuwa maendeleo
hayawezi kuja ikiwa miundombinu ni mibovu hivyo atahakikisha
analifikisha kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi
hyo ifanyike mapema.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa
CCM,mapema leo jioni katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi.Kinana
alisema kuwa, Serikali inatambua matatizo ya wananchi wa kjijini hapo
ikiwemo suala la pembe jeo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi. "Miradi
yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwakua wote ni
watanzania"alisema.Alisema kuwa Serikali inatambua kuwa shughuli kubwa
ya kijini hapo ni uvuvi hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa
kuwasaiidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi ili waweze
kujiendeleza.
Mdau
Kamanda wa Matukio Richard Mwaikenda akitafuta taswira mwanana kabisa
kwenye mkutano wa hadhara mapema leo mchana katika kijiji cha
Kabwe,wilani Nkasi mkoani Rukwa.