SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari wa Jeshi la Polisi
aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 na picha
yake kudaiwa ‘kuminyiwa’ na askari wenzake ili isionekane, hatimaye imepatikana
Mwanamama
ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca
Kilwai mwenye namba WP 5367 anayedaiwa kuiba mtoto wa jinsia ya kiume
aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe (siku 7).
Askari huyo ambaye kituo chake ni Ilala jijini Dar, alikamatwa kwa
tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la
Goodluck Salehe (siku 7) aliyeibwa April 6, mwaka huu huko Kasumulu Kata
ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Ilielezwa kuwa, mtuhumiwa alishirikiana na baba mzazi aliyefahamika
kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela
aliyemtambulisha kwa mama mzazi (Mboka Mwakikagile umri miaka 20) kuwa
Prisca ni shangazi yake hivyo amekwenda kumwona mtoto aliyezaliwa ndipo
akatoroka naye.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 17, mwaka huu huko eneo la Meta
Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi
ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa Makao Makuu ya Polisi Mkoa Forest
ya Zamani kwa mahojiano zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku hiyo mama huyo alikuwa katika
harakati za kutokomea kusikojulikana lakini bahati nzuri polisi
waliimarisha ulinzi.
“Alikuwa ndiyo yupo katika mikakati ya kutoroka na haikujulikana
alikuwa anataka kwenda wapi maana tayari alishajua kuwa anatafutwa hivyo
kutapatapa na kuingia kirahisi katika mkono wa sheria,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kuhojiwa na polisi kujiridhisha na tuhuma hizo za wizi,
mstakiwa huyo alipandishwa katika mahakama ya…na kusomewa mashtaka
yanayomkabili.
Baada ya kusomewa mashtaka siku hiyo, kesi iliahirishwa hadi Mei 6,
mwaka huu ambapo mshtakiwa aliruhusiwa kupata dhamana lakini akashindwa
kutimiza masharti (wadhamini wawili na hati) hivyo kurudishwa sero hadi
kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kabla ya kunaswa katika tukio hilo,
askari huyo anayedaiwa kuwa ni mama wa watoto, aliolewa na kuachika
miaka kadhaa iliyopita.
chanzo: gazeti ijumaa wikienda
