PICHA 6 ZA AJALI YA BASI LA URIO ILIYOTOKEA LEO KIA MKOANI KILIMANJARO


 Wananchi wakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruhiwa.
 Picha juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye  basi hilo aina ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai  mkoani Kilimanjaro
 
Basi aina ya Urio yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea  Leguruki mkoani  Arusha leo limepinduka katika eneo la Kia na kujeruhi watu zaidi ya 31.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani.
"Dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama barabara ndipo ilipo anguka gafla  na kubiringita mara tatu apa yenyewe unavyoiyona tumeigeza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina.
 
 Mpaka kamera ya libeneke la kaskazini inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya Leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya pasaka 

-LIBENEKE LA KASKAZINI
 
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo