ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto-Tanga wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa basi jingine katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio,inaeleza kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha wakati magari hayo yakijiandaa kuanza safari mara baada ya kuzuiliwa kwa muda kupisha msafara wa Rais Kikwete.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.
Juhudi ya kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha idadi kamili ya waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo
Tutaendelea kujilishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.

Chanzo:Michuzi media