ALIYEKUWA
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anatarajia kuwa mgeni
rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Mei 4 Jijini
Mwanza.Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era kamati imejipanga kufanya tamasha la kishindo jijini humo kwa sababu maandalizi yake ni ya hali ya juu.
Mang’era
alisema tamasha hilo litakuwa ni la aina yake ambako alitoa wito kwa
wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Mang’era
alisema sambamba na Ngeleja, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen
Masele anatarajia kuwa mgeni rasmi mkoani Shinyanga Mei 3. Aidha Mang’era alisema
mipangilio ya kuelekea tamasha hilo inaendelea vizuri hivyo wakazi wa
Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula kupata neno la Mungu kupitia waimbaji
mbalimbali wa Tanzania na nje.
Alisema
tamasha hilo jijini Mwanza linatarajia kukongwa na muimbaji raia wa
Afrika Kusini, Rebecca Malope na wengineo watakaoteuliwa na kamati ya
maandalizi.