Na
Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania
ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika
lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) . Kauli
hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada
huo ambao utatumika kukuza sekta ya
kilimo na kupunguza umasikini nchini. Katibu
Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA)
ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo
wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu
Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali
inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri watanzania
takribani asilimia 74 nchini. Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya
Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda
kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa
upande wake Balozi wa Japan nchini
Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga
zaidi sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko
ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo. Naye
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano
mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu
mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo
katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru
Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini
Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu
Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi
kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini. Serikali
ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo inaongozwa
na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo
itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini
nchini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano
ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo
uliotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA)
leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala
ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia)
ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA)
leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba
uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini
mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam. (Picha
zote na Eleuteri Mangi).
========= ========= =========