MWANAMKE AMCHOMA KISU HADI KUMUUA MWANAUME ALIYETAKA KUMBAKA

Wakati wakristo na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kote duniani wakiendelea kusherehekea sikukuu ya pasaka hali imekuwa tofauti katika familia ya bwana Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga kufuatia  kuuawa kwake kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja (jina tunalo mwenye umri wa miaka 24)katika eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla ameuambia mtandao huu  kuwa tukio hilo limetokea Aprili 20,mwaka huu saa tisa usiku.

Amesema  siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani,akafariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi.
 
chanzo:malunde1 blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo