Wanawake
watatu wasiojulikana majina yao wamemtapeli mwanafunzi wa Chuo cha Jiji
la Dar es salaam (Dacico), Monica Crispin simu nne zenye thamani ya
Sh145,000 baada ya kumdanganya kwamba watamsaidia kusafisha nyota ili
fanikiwe katika maisha yake.
Mwanafunzi
huyo alisema kwamba alikutana na matapeli hao karibu na lango la chuo
na mmoja wao alimwomba aelekezwe kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Mama
John.
Monica
alisema alimjibu kwamba hamfahamu na ghafla alijitokeza mwanamke wa
pili aliyejifanya anamfahamu Mama John na kumtaka Monica aongozane nao
ili akawaonyeshe.
Alisema
alikubali kuwaongoza, lakini baada ya dakika chache mmoja wao
alimwambia kuwa wao ni wasafisha nyota na wanataka kumsaidia. “Walinitaka
niwapatie kiasi chochote cha fedha, lakini nilipowaambia kwamba sina,
wakanishauri niwape simu hata kama ni nne au zaidi ili wazisafishe
nyota,” alisema.
Monica
alisema katika mazingira ambayo hakumbuki, alijikuta akikubali kila
kitu na hatimaye alikwenda darasani kuwaomba wanafunzi wenzake wampe
simu ambazo alizipeleka kwa wanawake hao.
Alisema aliwapelekea simu wanawake hao na baada ya kupata simu hizo walimtoroka.
Baada
ya kutapeliwa alikwenda moja kwa moja nyumbani ambako alimweleza mama
yake ambaye alifika naye shuleni na kuwalipa wanafunzi wote waliokuwa
wakimdai simu mwanafunzi huyo
