MTABIRI HASSAN YAHYA HUSSEIN ATABIRI DIAMOND NA WEMA WATAFUNGA NDOA AGOSTI MWAKA HUU

MTABIRI mwenye jina kubwa kwa sasa Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Yahya Hussein ameibuka wiki hii na kuanika kwamba, Agosti mwaka huu Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu watafunga ndoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzikati, Hassan alisema amepiga mahesabu ya kinyota kwa wapenzi hao na kubaini kuwa, Agosti ndoa yao itafungwa mahali popote nchini Tanzania.

Akaongeza: “Kama wapo kwenye mipango au maandalizi wakazane, kwani mwezi Agosti ndiyo wenyewe kwa mujibu wa nyota za wote.

“Lakini nawapa angalizo muhimu, wakae wakijua kwamba kama ndoa hiyo haitatimia Agosti kutokana na sababu zao wenyewe, haitafungwa tena hadi mwaka 2016, kwa sababu lazima ndoa yao iwe kwenye mwaka unaogawanyika.”

Maalim Hassan aliendelea kuweka wazi kwamba, vikwazo vyote ambavyo vilikuwa vikiwazunguka wawili hao, kwa mujibu wa nyota zao, vimetoweka, akimaanisha havipo tena.
 
Chanzo: Amani


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo