Kamati ya Tanzania kwanza ya Nje ya Bunge Maalum la Katiba jana wametoa ya moyoni mbele ya waandishi wa habari juu mwenendo mzima wa Bunge maalum la Katiba baada ya kutoridhishwa na kuonyesha ni kwa jinsi gani wajumbe hawana mapenzi ya dhati ya kutengeneza Katiba mpya.
Augstino Matefu ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Tanzania kwanza
alianza kwa kusema:
"Ukiangalia wajumbe wengi wameweka maslai ya vyama na Taasisi zao na si Nchi kwani inaeleweka wazi mada ya kudai Katiba mpya ilibebwa na baadhi ya Vyama vya Siasa na Taasisi Fulani kwa lengo kudai muundo mzima wa kuunda Tume huru ya Uchaguzi"

"Lakini cha kuchangaza watu hawa wameona na kukubali kutumiwa na
Mataifa na Nchi za Mataifa ya Magharibi kwa lengo la kuigawa Nchi yetu
vipande vipande na kwa lengo la kundi kutawala tena hususani kwa upande
wa visiwa vyetu wakiamini havina ulinzi na usalama mathubuti"
Kingine
walichokizungumza ni kuhusu Profesa Lipumba ambapo walisema:
"Kwa mfano Mh Prof Lipumba alipopokea taarifa za kuungwa mkono na baadhi ya Nchi ya Magharibi aliweza kufuata msimamo wake na kupinga makala aliyoitoa ya kuunga mkono muundo ulio asisiwa na hayati Mzee J.K. Nyerere na Mzee Karume."

Hii ni ratiba ya Maandamano na Mikutano ya Hadhara itakayofanywa kikanda na Kamati ya Tanzania kwanza nje ya Bunge.
- KANDA YA KASKAZINI (ARUSHA MH. DR HALSON MWAKYEMBE NA SIXTUS MAPUNDA)
- NYANDA ZA JUU KUSINI (MBEYA MH. PROF MWANDOSYA NA NDUGU ASENGA)
- KANDA YA MAGHARIBI (KIGOMA MH. MWIGULU NA IDDI MAJUTO)
- KANDA YA KATI (DODOMA NA TABORA MH. SAID NKUMBA)
- KANDA YA KUSINI (MTWARA MH. PANDU AMIR KIFICHO)
- KANDA YA MASHARIKI (DSM MH. NAPE NA MH. ABBAS MTEMVU)
- KANDA MWANZA (MH. PAUL MAKONDA NA NDG MATEFU)
- ZANZIBAR (PEMBA MH. HAMAD RASHID NA MH. RENATUS MHABI- KATIBU MKUU CCK (CHAMA CHA KIJAMII).
- UNGUJA (MH. MASAUNI NA MH. JUMA K. SADIFA (KIBANDAMAITI