WAFANYAKAZI wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi
‘STRATBAG’ iliyopo maeneo ya Ubungo jijini Dar, leo asubuhi wameingia
katika mgomo wakipinga uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa mishahara midogo
wafanyakazi wake na kuondolewa posho zao za wiki na mwisho kabisa
wakipinga suala la kutopewa ajira kwa vibarua waliofanya kazi kwa muda
mrefu katika kampuni hiyo.
Kamera yetu ilifika eneo la tukio na kuwamulika wafanyakazi wakiwa
wamekaa bila kujishughulisha na kitu chochote wakisubiri muafaka kutoka
kwa viongozi wao ambao hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio
hakukuwa na muafaka wowote uliofikiwa baina ya mabosi wa kampuni hiyo na
wafanyakazi.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)