HUU NDIO WIMBO KUHUSU MUUNGANO ULIOWAKUTANISHA WASANII 50 WA TANZANIA, USIKILIZE HAPA

Wimbo Maalumu wa Muungano ulioimbwa na wasanii 50 kutoka Tanzania ambao kwa pamoja walikaa na kutengeneza wimbo huu,jina la wimbo huu unaitwa Tuulinde umetayarishwa na maproducer wawili Ema the boy na Tuddy Thomas kutoka Soround Sound Studio.
 
Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki wa hapa Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili.

Inawezekana ikawa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.

Miongoni mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni pamoja na Kadjanito, Mwasiti, Linah, Christina Shusho, Khadija Kopa, Frola Mbasha, Ommy Dimpoz, Diamond, Josse Mara, Kalala Jr, Ali Kiba, Peter Msechu, Mrisho Mpoto, Abdul Kiba, Mzee Yusuph, Angel, Mwana Fa, Nikki Wa pili, G Nako, GodZilla, Madee, Asley, Shaa, Mandojo, Domokaya, Shilole na Roma Mkatoliki.
Bonyeza play kusikiliza wimbo huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo