-
Akitoa taarifa hiyo mbele ya Bunge maalumu la katiba, Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalumu, Mh. Pandu Amiri Kificho alisema;
“Waheshimiwa wabunge taarifa inasomeka kama ifutavyo;
Taarifa
ya upotoshaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Mh. Paul
Makonda, anahojiwa na vyombo vya usalama vya Bunge kwa tuhuma za wizi wa
simu.
(Sasa
Kitengo cha usalama chetu ambacho hicho kinachotegemewa ndiyo
kinamuhoji, kinatoa taarifa hii,ili kuweka wazi na kuondoa hiyo tuhuma
ya upotoshaji iliyotolewa)
Mnamo
tarehe 27/02/2014 kwenye vyombo vya habari hususani kwenye mitandao ya
kijamii, zilitolewa taarifa kwamba Mh. Paul Makonda anashikiliwa na
vyombo vya usalama vya Bunge kwa mahojiano kutokana na tuhuma za wizi wa
simu ya mjumbe mwenzake ndani ya ukumbi wa Bunge. Mtoa taarifa kwenye
mitandao hiyo alieleza kwamba, wakati anatoa taarifa yake Mh. Paul
Makonda, alikuwa chini ya ulinzi akipekuliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za
wizi huo.
Kitengo chetu kinasema ukweli ni kwamba, taarifa hiyo ni ya uongo (makofi) na yenye nia ya kumchafua Mh. Paul Makonda (makofi) pamoja na taswira mzima ya Bunge Maalumu. Mh. Paul Makonda ambaye ni mjumbe wa Bunge hili maalumu hana tuhuma yeyote inayohusiana na wizi wa kitu (makofi) chochote ndani ya maeneo ya Bunge hili maalumu, tangu ajisajiri kama mjumbe wa Bunge hili maalumu na wala hajawahi kupekuliwa na kutuhumiwa (makofi) kwa kosa lolote la aina hiyo na hivyo hashikiliwi wala haojiwi na chombo chochote cha usalama wa Bunge (makofi).

Waheshimiwa
wabunge naomba niendelee kukemea, kwa mambo ya namna hii, ambayo
yanachafua Mjumbe mmoja mmoja na hatimaye kuchafua Bunge hili maalumu
lenye heshima kubwa (makofi). Tuwaombe wote wenye mitandao ya kijamii,
lakini na vyombo vingine vya habari vyote tuache mtindo huu. Tuache
mtindo huu, ni mambo ambayo yanaweza kumpa nafasi yule, ambaye anazuliwa
kwa tuhuma za uongo wa aina hiyo, hata kuweza kufungua mashtaka akiona
inafaa (makofi).
Hii ni kwa yule atakayekuwa ametuhumiwa, lakini bado kwa kutuhumiwa mjumbe mmoja wapo, kwa taarifa za uongo za aina hii, hii inachafua heshima ya Bunge hili (makofi). Kwa hiyo, niiombe mitandao hiyo ya kijamii, niombe vyombo vya habari, Televisheni na Radio hata wale wanaoandika kwenye magazeti mbalimbali kwamba jambo hili hatutaki litokee kwa mara nyingine tena (makofi). Tujitahidi sana, tuwe tunatoa taarifa zenye ukweli ambazo zitakua na maana kwa jamii yetu ya Tanzania. Jambo hili tuachane nalo, halifai, lisituchanganye na kutuvunjia heshima zetu wajumbe lakini pia Bunge hili maalumu tukufu.

Nawashukuru sana kwa hilo”