Sheikh wa Msikiti MKuu wa Bondeni, Mustapha Mohamed Kiago (49) na mwanaye Khalid Mustapha (10) wanasadikiwa kumwagiwa tindikali, wanaendele vema.
Wawili hao, wamelazwa kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa
matibabu, baada ya kumwagiwa kimiminika hicho, hivyo kujeruhiwa shingoni
na usoni.
Akizungumza nasi kwa njia ya simu ya kiganjani Jumamosi jana,
Sheikh Kiago alimshukuru Mungu, kwani afya zao zimeimarika na hali ya
mwili `kuchoma-choma’ imepungua.
"Lakini bado tupo wodini na sasa afya zetu zimezidi kuimarika na
hasa mtoto wangu ambaye alikuwa hawezi kufumbua macho kwa jana, ila leo
anaweza kuangalia," alisema Kiago.
Alisema kutokana na hali ya mtoto wake kuwa mbaya kwa jana, alilazimika kuhamia wodi ya watoto.
Juzi, Sheikh huyo na mwanaye walilazwa hospitalini hapo baada ya
kumwagiwa tindikali na mtu asiyefahamika, wakati wakiingia msikitini
kuswali.