Msanii wa filamu za Kiswahili, Aunt Ezekiel ambaye
anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa Bongo Flava alioupa jina la ‘Mguu
kwa Mguu’ aliomshirikisha Linex Mjeda, ameeleza sababu kubwa iliyomfanya
aingie kwenye game la Bongo Flava.
“Unajua game la Tanzania linabadilika badilika kwa hiyo nimeona ngoja
pia nijihusishe katika uimbaji ili niendelee kuteka mashabiki, mimi
zamani nilikuwa napenda sana Bongo Flava na sio kwamba nilikuwa naimba
hapana, nilikuwa kama nikiona wasanii wakianza kuimba basi moyoni
nafurahi sana. Siku moja wakanipa ushauri na hapo ndipo nikaingia studio
na kutengeneza wimbo wa ‘Mguu kwa Mguu.” Aunt Ezekiel ameiambia tovuti
ya Times Fm.
Ameeleza kuwa alitegemea kuachia wimbo huo mwaka jana ila ratiba zake hazikwenda vizuri hivyo aliamua kuiachia rasmi mwaka huu.
Mguu kwa Mguu ni wimbo uliotayarishwa na Mr. T Touch ndani ya Seductive Records .