Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kulia) akitoa agizo hilo kwa mkuu wa kituo cha polisi Kahama Elias Haway na mkuu wa Upelelezi Wilaya Twaha Juma. |
Mkuu
wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, ameliagiza jeshi
la polisi wilayani humo kumtafuta na kumkamata Afisa Mtendaji wa Kata ya
Mega, Peter Kupingwa, kwa tuhuma za kuhusika katika kumtorosha mkulima
wa Bangi.
Mpesya
ametoa agizo hilo jana baada ya kufika katika shamba lililokuwa
limelimwa bangi hiyo lililopo katika kijiji cha Masabi, huku akiwa
ameongozana na askari polisi na kukuta bangi hiyo imeshavunwa na kubaki
miche kadhaa iliyochukuliwa kama ushahidi.
Imedaiwa Afisa mtendaji huyo alitoa agizo la kuachiwa kwa Mtuhumiwa Juma Maliatabu ambaye juzi alikamatwa na sungusungu baada ya Afisa Kilimo wa kata hiyo Edwin Kasaba kuwapa taarifa za kukuta zao hilo katika shamba la Malingita.
Baaadhi ya miche ya bangi iliyopatikana katika shamba hilo ikiwa imeshikwa na askari poliSI. |
Mpesya
ametaka kukamatwa kwa Kupingwa ambaye ni mwajiri wake kutokana ma
kuonesha kukerwa na kitendo alichokifanya cha kutetea na kuendelea
kuwakumbatia watuhumiwa na kuongeza kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Shamba hilo la Hekari moja na nusu limelimwa mahindi huku yakiwa yamechanganywa na zao la Bangi ndani yake, jambo lililomfanya Afisa kilimo kwenda kukagua kama sehemu yake ya kazi kutembelea mashamba ya wakulima na kutoa ushauri.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Shamba hilo linamilikiwa na Ndugu wawili Juma Maliatabu na Malingita Maliatabu ambaye pia hadi sasa hajulikani alipo baada ya kukosekana katika msako huo wa Polisi ambao bado unaendelea.
Hata hivyo Jeshi la wilaya ya Kahama lililokuwa likiongozwa na Mkuu wa kituo cha polisi Kahama Elias Haway na Mkuu wa Upelelezi Wilaya Twaha Juma limefika katika kaya za Watuhumiwa kwa lengo la kuwakamata bila Mafanikio.

NA DUNIA KIGANJANI