MKUU WA MKOA WA NJOMBE ATENGUA MAAMUZI YA BARAZA LA MADIWANI WANGING'OMBE

 
Mkuu wa mkoa wa Njombe capteni Mstaafu Asseri Msangi Akitengua maamuzi Hayo Kwenye Kikao na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari Wakiendelea na Kazi Yao Kwenye Kikao Hicho
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi  Ametengua Maamuzi ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Lililoridhia Maombi Ya Wataalamu wa Halmashauri Hiyo Kuhamia Katika Majengo ya SIDO Yaliyopo Mjini Njombe Kutokana na Kutokamilika Kwa Ofisi Katika Halmashauri ya Wanging'ombe.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Ofisini Kwake Mkuu Huyo wa Mkoa Capteni Mstaafu Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Baraza Hilo la Madiwani Kuridhia Maombi ya Watendaji Hao Pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Amelazimika Kutengua Maamuzi Hayo Kwani Serikali Iliagiza watendaji na wataalamu wote Kuhamia Igwachanya.

Amesema Kuwa Kitendo cha Mkurugenzi na Wataalamu Wake  Kuhama Igwachanya Ambako Ndiko Makao Makuu ya Wilaya Ya Wanging'ombe na Kuhamia Njombe ni Kukiuka Agizo la
Rais Pamoja na Waziri Mkuu Aliyeagiza Watumishi Wote Kuhamia Huko.

Amesema Katika Ziara Yake ya Hivi Karibuni Aliyoifanya Katika Wilaya za Ludewa,Makete na Wanging'ombe Amebaini Kuwepo Kwa Changamoto Mbalimbali na Kuwaagiza Viongozi wa Ngazi Mbalimbali Kushughulikia Changamoto Hizo Zikiwemo za Sekta ya Elimu,Maji na Umeme.

Katika Hatua Nyingine Keptein Mstaafu Msangi Ameagiza Kila Halmashauri Kuunda Kamati Itakayosimamia Suala la Mchakato wa Ufikishaji Nishati ya Umeme Vijijini Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA Ili Kuendana na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2010/2015.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo