
Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupata habari ya ndege ya Malaysia imeanguka kwenye bahari ya Hindi.
Shirika
la ndege la Malaysia Airlines leo Jumanne limesema limetoa $5,000
ambazo ni takriban shilingi milioni nane kwa ndugu waliofiwa kufuatia
ajali ya ndege yake ya MH370. Fedha hizi ni kwa kila abiria aliyekuwa
kwenye ndege hiyo.