Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Godfrey Mgimwa (32), akilakiwa kwa shangwe na vigeregere alipowasili
katika Kijiji cha Magubike, Kata ya Nzihi, Iringa Vijijini, kufanya
mkutano wa kampeni leo mchana
Wafuasi
wa CCM wakishangilia kwa nguvu wakati Mgimwa akihutubia kuwaomba
kura.Uchaguzi wa Jimbo hilo la Kalenga utakuwa Machi 16, mwaka huu.
Mfuasi
wa CCM, akishangilia kwa furaha baada ya kufurahishwa na hotuba nzuri
ya Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha
Magubike.
Mgimwa
akiwa maebebwa na wafuasi wa CCM alipowasili katika mkutano wa kameni
katika Kijiji cha Ilalasimba, Kata ya Nzihi, Jimbo la Kalenga leo
asubuhi.
Ni nderemo kila mahali katika mkutano wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Ilalasimba
Kaimu
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akimnadi kwa wananchi
mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika
Kijiji cha Ilalasimba leo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba akihutubia mkutano
wa hadhara kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Gofrey Mgimwa katika
Kijiji cha Magubike.