Mtangazaji
wa Channel Ten, Salum Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo
alikuwa akiendesha kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro.
Kwa mujibu wa
mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten, Mkambala alipata ajali hiyo maeneo ya Chalinze alfajiri
ya leo na hali yake inaelezwa kuwa ni mahututi baada ya kuumia vibaya.
Haijafahamika yuko hospitali gani kwani alikuwa peke yake kwenye gari na
taarifa ilitolewa na msamaria mwema kwa simu ya Salum na baada ya hapo
simu yake
haipatikana tena.
CHANZO: GPL