Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Halmashauri za Mkoa wa Njombe Zimeshauriwa Kujikita Katika Suala la Upimaji wa Ardhi Kwenye Maeneo Yao Hususani Kwenye Miji Kama Moja ya Njia ya Kuongeza Mapato Ya Ndani Kupitia Kodi ya Ardhi.
Ushauri Huo Umetolewa Hivi Karibuni na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau Kufuatia Kuwepo kwa Maeneo Ambayo Hajapimwa Yakiwemo Maeneo Mapya ya Kiutawala.
Bwana Saitabau Amesema Kuwa Maeneo Yanayopaswa Kupewa Kipaumbele Zaidi Katika Zoezi la Upimaji ni Pamoja na Maeneo ya Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe Igwachanya, Maeneo ya Vijiji na Miji, na Kuongeza Kuwa Wananchi Wanapaswa Kuwa na Umiliki Halali wa Ardhi.
Aidha Katibu Tawala Huyo Amesema Endapo Wananchi Watakuwa na Hati Miliki za Ardhi Zikiwemo za Kimila Itawarahisishia Katika Udhamimi wa Shughuli Zao Ikiwa ni Pamoja na Kupata Mikopo Kutoka Taasisi za Kifedha.
Mkoa wa Njombe Umeendelea Kuzihamasisha Halmashauri za Wilaya Kuwapima Maeneo Kwa Ajili ya Wananchi Wake Lakini Bado Kuna Changamoto Kwa Baadhi ya WananchiKutopimiwa Maeneo Yao Kutokana na Sababu Mbalimbali Zikiwemo za Kiuchumi.