DARAJA
la MTAMA Llilokatika Tarehe 26/3/2014 na kuzuia mawasiliano ya barabara
kati ya lindi na newala kwenda Tandahimba mkoani Mtwara.Baadhi ya abiria walionasa kufuatia kukatika kwa daraja Nyangao wilayani Lindi kutokana na Mvua zinazoendelea
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ilkiongozwa na mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa
Lind, Ludovick Mwananzila ilipofika eneo la Nyangao kukagua athari za
Mafuriko hayo.Mmoja
wa abiria aliekwama baada ya kukatika kwa daraja la Nyangao
linalounganisha barabara ya lindi na masasi kwenda Nachingwea na Tunduru
akijaribu kuvuka mara baada ya kutengeneza njia ya muda kunusuru abiria
kutokana na mafuriko yaliyotokea Tarehe 26/3/2014.Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akiithibitisha njia ya muda mara
baada ya kukatika kwa daraja la mto Nyangao lililokatika jana, Kulia ni
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga waliofika kukagua athari
zilizojitokezaBaadhi ya abiria wakivuka katika daraja la Nyangao Lindi picha na Abdulaziz Lindi
Na. Abdulaziz Video, Lindi
Mafuriko yaua na kusitisha usafiri Lindi Masasi,Ruangwa na Nachingwea ikiwemo Newala na Tandahimba Mkoani Mtwara
Watu Wanne wamefariki dunia katika wilaya ya Lindi kutokana na mvua
zilizonyesha usiku wa Tarehe 26 na 27 /3/2014 na kusababisha mafuriko
makubwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Lindi, Nachingwea na
Ruangwa Mkoani Lindi
Sambamba
na mvua hizo licha ya kupoteza maisha ya watu hao na wengine kujeruhiwa
pia Imesitisha huduma za usafiri kati ya Lindi, Masasi, Nachingwea,
Ruangwa na Newala kufuatia kukatika kwa madaraja ya Mtama na Nyangao
pamoja na makazi ya wananchi wanaoishi pembezoni kulikosababishwa na
kufurika kwa mto Lukuledi.
Akiongea
na globu hii mara baada ya kukagua athari hizo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
Ludovick Mwananzila alieleza kuwa Tayari Wakala wa barabara Mkoa wa
Lindi inafanya jitihada za haraka kuweka njia ya Muda ili kuokoa
wananchi wengi waliokwama katika maeneo hayo ili kupunguza msongamano
uliopo Sambamba hilo Mwananzila alitoa wito kwa baadhi ya wananchi
waliopo maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo kutoruhusu watoto wao kucheza
katika mto huo kutokana na ongezeko kubwa la maji.
Aidha
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi aliwahakikishia usalama abiria wote
waliokutwa na maafa hayo kuwa Jeshi la polisi limejipanga kutoa ulinzi
wakati wote katika maeneo hayo huku akitoa agizo kwa wenye mabasi ya
Abiria kutofanya safari hadi kutakapokamilika kwa maeneo hayo ili
kupunguza idadi kubwa ya wasafiri.
Kukatika
kwa madaraja hayo tayari kumesitisha Usafiri kwa wanaotoka Mkoa wa
Lindi kwenda wilaya za Masasi, Nachingwea, Tunduru, Ruangwa, Liwale,
Nanyumbu, Newala