Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ametoa changamoto kwa wajumbe
wenzake wanawake walio kwenye Bunge hilo, kujenga hoja zenye nguvu
zinazohusu masuala yanayohusu wanawake na kuzitetea kwa sauti moja ili
ziweze kupita katika Rasimu ya Katiba.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mhe. Anne ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa mchango wake kwa wajumbe wa
semina ya kujenga agenda muhimu kwa masuala ya kijinsia iliyoandaliwa na
Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(TWPG) kwa wajumbe wanawake wa Bunge hilo, iliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Pius Msekwa.
“
Ninawaomba tuwe na hoja zenye nguvu wakati wakuchangia mjdala wa
Rasimu ya Katiba . Tukisimama kwa hoja za nguvu na kutetea vifungu
vinavyohusu masuala ya wanawake tunaweza kubadilisha vifungu.
Tuzungumzeni hoja tuache kufanya fujo, tusiingie katika malumbano ambayo
hayana tija, tuache kuzomea tukifanya hiyo tutakuwa tumejijengea
heshima,” alisema Mama Anne.