Kijana
Zakaria Ulaya amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tabora
mjini akituhumiwa kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa Shule ya msingi
Gongoni tukio ambalo lilifanyika huko kata ya Ipuli manispaa ya
Tabora
Akisomewa maelezo ya kosa Zakaria amekana kuhusika na tukio
hilo,hata hivyo amerejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutekeleza
masharti ya dhamana ambapo walihitajika watu wawili ambao wangeweza
kumdhamini kwa fedha zenye thamani ya shilingi milioni tatu kila
mmoja.
Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 12 March mwaka huu.
chanzo
kapipij blog