Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali amefunguka na kudai kuwa yeye mzuka wake kimapenzi upo kwa wanaume weusi na sio wanaume weupe.
Kupitia kipindi cha Leo tena February 28, Wema Sepetu amekubali
kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali
lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa
gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio
shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini
nisimpende”
“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa
kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na
utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na
imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa
sasa tumeamua kuwa serious’.