AFARIKI DUNIA BAADA YA KULIPUKIWA NA PETROLI TARIME

Watu watatu wamekufa wilayani Tarime katika mazingira tofauti akiwemo anayeuza mafuta ya petroli kwa vidumu.
Muuza petroli huyo, Itembe Gabriel Itembe (36) alilipukiwa na mafuta wakati akimpimia mafuta mteja wake huku akiwasha kibatari.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya Kamishina msaidizi, Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 22 usiku katika Kijiji cha Borega tarafa ya Inchage.

Kamanda Kamugisha alisema kwamba Machi 24 mkazi wa Kijiji cha Ziba Wilaya ya Igunga  Tabora aliyefahamika kwa jina Masele Mathias ( 28) alidondoka na kufa kutoka kwenye lori lenye namba za Usajili T 531 ASB likivuta tela  namba T 128 AWP.

Ajali hiyo ilitokea kijiji cha Makongoro kata ya Rabuor katika barabara kuu itokayo Mwanza kwenda Sirari na Kenya.

Katika tukio jingine, mwili wa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umrikati ya miaka 38 na 40 uliokotwa vichakani katika kijiji cha Kangariani kata ya Itiryo tarafa ya Ingwe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo