SOMA TAARIFA KUHUSU KALA JEREMIAH KUNUSURIKA KIFO KWENYE AJALI MBAYA YA GARI

kala-ajaliLeo Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha inayoonyesha ajali aliyoipata wakati akitokea kwenye show yake iliyokuwa ikifanyika Club East 24 ambayo alikua akifanya show pamoja The B Band ya Banana Zoro.

Hiki ndicho alichokipost Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Screenshot_2014-02-15-14-35-32 
Chini ya Post ya picha ya gari yake Kala aliandika maneno haya>>nIMEPATA AJALI USIKU HUU NIKIWA NATOKEA CLUB EAST 24 AMBAKO NILIKUWA NAFANYA SHOW NA B BAND WAKATI NARUDI NYUMBANI GHAFLA KUNA MTU WA PIKIPIKI AKAWA ANATAKA KUINGIA NIKAJARIBU KUMKWEPA GARI ILIKUA MWENDO KASI KIDOGO IKAYUMBA KWENDA KULIA NIKAIRUDISHA IKARUDI ZAIDI KUSHOTO NIKAIRUDISHA TENA KULIA IKAWA INATAKA KWENDA MTARONI NIKAIRUDISHA TENA KUSHOTO AMBAKO ILIGEUKA ILIKUKUA INATOKA NA KUINGIA MTARONI AMBAKO ILIKITA NA KUVUNJA MLANGO WA UPANDE WANGU.SIJAAMINI KAMA NIMETOKA BILA HATA JERAHA MGUUNI WALA MAUMIVU ZAIDI YA YALE UA KICHWANI KIDOGO NILIYOJIGONGEA KWENYE MLANGO KWA JUU.AHSANTE SANA MUNGU UMENIOKOA.ASANTE SANA MUNGU WANGU.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo