BIASHARA ya dawa za kulevya mjini
Iringa inaendelea kutafutiwa muarobaini, baada ya juzi, jeshi la polisi katika
msako wake, kumkamata mtu mmoja akiwa na dawa hizo.
Mtu huyo, Vasco Kitosi, alikamatwa akiwa na gramu 50 za bangi ambayo ni aina ya dawa za
kulevya inayoelezwa na wanahakati wa mapambano ya matumizi ya dawa hizo, kutumiwa
na vijana wengi mjini Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Iringa,
Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo linalomuhusisha kijana
huyo mwenye umri wa miaka 21.
source; http:frankleonard.blogspot.com
