Mkuu wa mkoa wa Njombe Aseri Msangi(kushoto) akizungumza na waalimu na viongozi wa kata na tarafa kuhusu sakata la baadhi ya vijiji kugoma kuchangia michango ya shule ya sekondari Mlondwe.Kulia ni mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro.
Diwani wa kata ya Mlondwe Alphonce Nkwama akisikiliza maagizo anayopewa na mkuu wa mkoa.
Mkuu wa mkoa akiendelea na kikao.
Mkuu wa mkoa wa Njombe akizungumza na wananchi wa kata ya Itundu katika mkutano wa hadhara.
===
Sakata
la vijiji viwili vya kata ya Mlondwe kusuasua kutoa michango kwa ajili
ya sekondari ya Mlondwe ambayo kwa sasa ipo kwenye kata mpya ya Itundu
wilayani Makete limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Njombe
Aseri Msangi kufanya ziara katika kata hiyo
Kutokana
na kusua sua huko mkuu huyo wa mkoa amemwambia diwani wa kata ya
Mlondwe Mh. Alphonce Nkwama kuwa anatakiwa kuwaeleza wananchi wake ambao
wanagoma kuchangia shule hiyo, serikali itachukua hatua ikiwemo
kuwaadhibu wale wote wanaogoma kuchanga
Akizungumza
na waalimu na viongozi wa kata na tarafa katika shule hiyo ya sekondari
Mlondwe Msangi amesema inasikitisha kuona hatua iliyofikiwa na wananchi
ya kuacha kuchangia michango ilihali watoto wao wanasoma shuleni hapo
si cha kiungwana hivyo wasipomaliza tatizo hilo, hatua zitakazochukuliwa
dhidi yao ni adhabu na wasiilaumu serikali
Amesema
mojawapo ya adhabu watakazochukua ni pamoja na kuwatoza ada mara mbili
au tatu ya ada ya kawaida inayolipwa na wazazi wanaochanga michango,
wazazi wote ambao hawachangi ili iwe fundisho kwao
"hatuwezi
kurudishwa nyuma na wananchi wazembe, dawa ni ndogo tu wazazi wote
ambao hawachangii watoto wao wakifaulu kuja hapa watalipa ada zaidi,
mfano kama mchango ni sh 10000/= wao watalipa 20000/= au 30,000/= au
zaidi ya hapo, tuone kama hamtazilipa kwa lazima" alisema Msangi
katika
hatua nyingine mkuu huyo akiwa katika kata ya Itundu na Mlondwe alipata
fursa ya kuzungumza na wananchi pamoja na kutembelea miradi ya maji
iliyopo katika kata ya Mlondwe