Taarifa kutoka Mtwara ambayo wana-amplify jeshi la polisi Mkoa wa
mtwara ni kuhusu mauaji yaliyotokea huko Mtwara ambayo chanzo chake
kimeelezwa ni wivu wa kimapenzi uliokuwepo kati ya wapenzi hao.
Jeshi la Polisi limesema mauaji hayo yametokea Ligula B kata ya
Ligula Tarafa ya Shangani mkoa wa Mtwara,ambayo yanamhusisha Habibu
Dastan au Upson Milanzi[26] ambaye anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Zuwena
Mwapindi[27].
Kifo cha Zuwena kinasemekana ni baada ya kuchomwa na kisu kwenye ziwa
lake la upande wa kushoto,mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo
alifanikiwa kutoroka lakini kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la
Polisi mkoa wa Mtwara wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa eneo
la Namayakata Tarafa ya Ziwani, Kata ya Nanguluwe, Wilaya ya Mtwara
vijijini.
Mtuhumiwa anategemewa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,
Mtandao huu umepata picha za marehemu lakini kutokana na sababu za kimaadili
hatutoweza kuziweka
credits:millardayo.com