Mambo yanazidi kuwa magumu kwa boss wa Watanashati Entertainment,
Ostaz Juma na Musoma baada ya kuweka picha ya PNC kwenye ukurasa wake wa
Facebook ikimuonesha msanii huyo akiwa amepiga magoti kumuomba msamaha,
kitendo kilichopondwa na kulaaniwa na wadau wa muziki.
Leo, ukurasa wa Facebook wa Ostaz Juma ulikuwa na ujumbe ulioonesha
kuwa amewaponda wasanii na watangazaji wa Tanzania kuwa wana njaa.
“Naona watu mmeguswa sana na mimi kuanika picha ya PNC katika
mitandao et, tatizo wasanii wa Tanzania mnanjaa sana kuanzia watangazaji
Radio na wasanii njaa ndizo zinazo wasumbua...” Hii ni ya kwanza ya maelezo yanayoonekana kuwekwa na Ostaz Juma kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Akiongea na Moko Biashara aka One B wa 100.5 Times Fm, Ostaz Juma
ameeleza kuwa watu wameiteka akaunti yake ya Facebook (hackers) na hivyo
hayo matusi yanayoandikwa sio yeye aliyeandika, na kwamba hali hiyo
inamfanya achanganyikiwe.
“Daah, nshachanganyikiwa rafiki yangu watu wamehack akaunti yangu
wanaandika matusi wanatukana watu..hadi hapa mimi nimeshachanganyikiwa
hadi hata kuongea siwezi bro. Unajua hapa Tanzania kuna watu fulani
hawataki watu fulani waendelee na wafanikiwe maisha yao. Hapa sasa hivi
wamehack akaunti yangu wameandika vitu ambavyo kwa mtu mwenye akili
timamu anajua kabisa Ostaz Juma hawezi kuandika vitu kama hivi.” Amesema
Ostaz Juma.
Ameeleza kuwa tayari watu hao walioiteka akaunti yake wamebadili
password na kwamba yeye binafsi hawezi kuingia na kuandika tena.
“Naomba tu watanzania waelewe kwamba mimi hiyo akaunti yangu
inayotumia jina la Ostaz Juma siitumii tena. Wamehack akaunti na
wamebadilisha password kwa hiyo hadi sasa mimi siko Facebook tena.”
Katika hatua nyingine, Ostaz Juma amesema kuwa tayari ameshamlipia
studio time PNC na amefanya wimbo na kwamba video ya wimbo huo
walishapanga utafanywa na kampuni ya Ogopa Videoz ya nchini Kenya.
Hata hivyo, baada ya kudai kuwa akaunti yake imetekwa na hackers, zimeanza kuonekana post nyingine akiomba radhi.
“NDUGU KWANZA KABISA NAOMBA NIWAOMBE RADHI KWA YOYE YALIYOTOKEA
NA KUBWA ZAIDI NI JUU YA POSTI AMBAYO ILIKUWEPO HAPA KWENYE ACCOUNTI
YANGU, UKWELI NI KWAMBA HAIKUWA POSTI AMBAYO MIMI BINAFSI NILIIANDIKA,
KUNA WATU WENYE NIA MBAYA NA MIMI WALI-HIKE AKAUNTI YANGU NA KUPOSTI
HICHO WALICHOANDIKA.. NAWAOMBA MNISAMEHE WALE AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA
NYINGINE WATAKUWA WAMEKWAZIKA NA POSTI HIYO, NASISITIZA KWAMBA HAIKUWA
POSTI YANGU NA NDIO MAANA NILIPOFANIKIWA KUIPATA TENA AKAUNTI YANGU
NIMEIFUTA NA KUANDIKA UJUMBE HUU.... SISI NI WATANZANIA NA NCHI YETU NI
YA AMANI NAMI PIA NI MPENDA AMANI, TUDUMISHE AMANI YETU.”
CHANZO: TIMES FM