Na Walter Mguluchuma,Mpanda Katavi
Mtu
mmoja alitambulika kwa jina la Richald Clavery 35 Mkazi wa Kijiji
cha Ikola Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda anashikiliwa na jeshi la
Polisi baada ya kukutwa akifukua kaburi la marehemu aliyefahamika
kwa jina la Tabu Omera
Kwa
mujibu wa kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Francis Maro
tukio hilo lilitokea hapo Februari 22 majira ya saa nne usiku
kijijini hapo nyumbani kwa Lenada Sakafu ambae alikuwa ni dada wa
marehemu huyo
Siku
hiyo ya tukio Lenada Sakafu alikuwa nyumbani kwake pamoja na
majirani na ndugu na jamaa zake wakiomboleza msiba wa mdogo wake
marehemu Tabu Omera aliyekuwa amefariki Dunia siku tatu kabla ya
tukio hilo kutokana na kushindwa kujifungua nakuzikwa nyumbani kwenye
eneo la nyumba ya Lenada
Alifafanua
kuwa mtoto wa Lenada aitwaye Brandina alitoka nje ya nyumba kwa
lengo la kwenda chooni kujisaidia ndipo aliposhituka kuona mtu akiwa
anafukua kaburi la marehemu mama yake mdogo
Alisema
hari hiyo ilimfanya Binti huyo arudi ndani ya nyumba na kutoa taarifa
kwa mama yake pamoja na majirani na ndugu waliokuwa ndani ya nyumba
hiyo
Watu
waliokuwa msibani hapo walishitushwa na taarifa hiyo nakulazimika
kutoka nje ya nyumba na waliweza kumkuta Richard Clavery akiwa
anafukua kaburi hilo la marehemu Tabu huku akiwa uchi akiwa amevua
ngu zake zote na kuzitundika kwenye msalaba wa kaburi hilo
Kaimu
kamanda Francis Maro alisema baada ya watu hao kumuuliza
anafanyanini hapo ghafla mtuhumiwa alishituka na akajifanya
kupandisha mashetani hata hivyo watu hao waliokuwa msibani hawakujali
walimkamata
Alisema
mtuhumiwa anatajiwa kufikishwa mahakamani ili aweze kujibu shitaka
la kufanya kosa la kufanya vitendo vya kishirikina