Mtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa kwenye pikipiki
Mtoto
Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Mkoani
wilayani Geita mkoani Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa
kamba na baba yake mzazi kisha kumfunga kwenye pikipiki na kuanza
kumburuza mtaa mzima kwa kutumia pikipiki hiyo.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika mtaa wa Mkoani ambapo inadaiwa kuwa binti
huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa
kwenda shuleni kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne
Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda
wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi majira ya saa 3 akiburuzwa huku
amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa
lengo la kumkamata bwana huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada
ya
kumtia mikononi walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo
Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea
mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya
wananchi kujaa hasira kali dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga hadi
waue lakini baada ya yeye kuwasiliana na polisi,polisi
walifika haraka na kumchukua hadi kituoni kwa usalama wake.
Afisa
upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na
kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa
upelelezi
zaidi.
Na Valence Robert-Geita